Promote your business for free grow your business for life you don't need to spend more money anywhere.

THIS BLOG IS SPONSORED BY AHADIWAY ,ADVANTAGES FOR JOINING AHADIWAY BOON CAREER (ABC) CHAPTER = Employment opportunities within and outside the country. , Job experience , Self -employment , Field stations, part time jobs and chances to be trained.

Friday, May 25, 2012

Waume za watu wananisumbua-Ushauri

"Da Nitonyeni, mimi na tatizo ambalo ni kama kwa kweli naona nimejitakia. Ni mdada au mama wa miaka 28 na nina watoto japokuwa tumetengana na mume wangu. Sasa unajua tena mijibaba(wanaume) wakishajua kuwa uko single wanaanza kukumendea.


Mimi tatizo langu ambalo lilisababisha kutengana na baba watoto lilikuwa ni uhuni wake, na nikaamua kumwacha ili tusije tukafa na UKIMWI na kuacha watoto. Na nikaapa sitakaa nitoke na mtu aliyeoa au sitakaa niharibu ndoa ya mtu kwa kuingilia penzi.


Sasa tatizo lilikuja hivi, mara nyingi sana mahali ninapofanya kazi waume za watu wanajaribu kunitongoza, na msimamo wangu nimekuwa sitaki kusikia mume wa mtu manake na mimi niliyaonja nilipokuwa kwenye ndoa yangu.


Sasa basi siku isiyoliwa kitu, kuna baba mmoja mume wa mtu kazini amekuwa akinisumbua zaidi ya wanaume wote ili niwe naye kimapenzi. Sasa siku moja tulikuwa na cocktail party na akaja na ushamba wake wa kunitaka kimahusiano, nami(jamani sijui kinywaji kilishaniingia) au ni shetani gani lilonifanya nifungue mdomo.


Nikamwambia kuwa mimi msimamo wangu ni ule ule 'sitaki kuwa naye' lakini kama anataka nimtafutie mtu basi nitafanya hivyo, he took up on the offer na kutokana nilikuwa na rafiki yangu wa kike ambaye ni single nikamwi-introduce.


Na baada ya wiki moja yule rafiki yangu niliyomwi-introduce akaniambia jamaa amenunulia sofa set, halafu mara wanafanya party ' na mara nyingi naona huyu jamaa ndio ana-finance' wananialika na zaidi ya yote inaonekana wamekuwa quite close katika uhusiano wao.


Mimi kama mwanamke ambaye nilishawahi kuolewa najisikia vibaya sana, yaani naji-picture kama mke wa huyu jamaa, naona kweli huyu baba ananyima familia yake upendo na anatoka nje na mimi ndie niliyefanya connection - yaani nimeshajilaaumu saaanaaa, najisikia vibaya kweli, hata kama ndugu wasomaji mkinitukana - kweli I deserve it - lakini yaani sijui jinsi gani yaku-reverse jambo hili. Sasa nimekuwa mbali na wote wawili, wakinialika kwenye party au kutoka nawapa excuse.


Mimi naomba......mnisaidie jinsi ya kufanya, japokuwa najua naweza kutoeleweka ( I risk to be misunderstood) wakadhania labda ni wivu etc, lakini ki ukweli ni kwamba - kujisikia kwangu vibaya ni kwa sababu nilikuwa kisaidizi kikuu kwa kuwakutanisha, na upweke wa mke wa huyu baba (wakati mume anajivinjari na kurudi nyumbani usiku, na uongo anaomwambia ili kuficha kinachoendelea) najua na naona ndio nimeusababisha - mimi naumia sana na mawazo.

Da Nitonyeni - nimeandika kwa ajili ya kutaka tu ushauri wa hali yoyote.
Nitashukuru sana."

Jawabu: Shukurani kwa kuniandikia. Kuna umri fulani mwanamke ukifikia wanaume wanaokutokea wengi wanakuwa tayari wamekwisha oa hiyo haina maana kuwa hakuna wanaume ambao hawana wake/wapenzi la hasha!


Wanawake wengi tunakutana na majaribu hayo. Mimi mwenyewe nakutana sana na vishawishi vya namna hiyo lakini as for me natumia nafasi hiyo kutaka kujua kwanini hasa huyo mume anataka kutoka na mimi hili hali anamke na watoto nyumbani, najitahidi kutafuta namna ya kujua ukweli wa nini anakikosa huko kwake na kutaka huku nje?......akiwa wazi nampa ushauri na ile kunitaka mimi kunabadilika na kuwa rafiki na mara mambo yakiwa mazuri unajikuta unatambulishwa kwa mkewe kama mtu uliyesaidia na sio "the other woman".


Ni kweli ulifanya kosa kubwa sana kuunganisha mume wa mtu kwa mwanamke mwingine ukijua wazi kuwa mwanaume huyo ana mke na watoto. Kama mwanamke mwenye maadili mema na mwenye kujali maisha bora kwa mwanamke mwenzio na watoto (ukizingatia kuwa wewe ni mama na sidhani kama ungependa watoto wako siku moja wateseke) ungemshauri mume huyo kutulia na mkewe.


Wakati mwingine unaweza kuokoa ndoa ya mwanamke mwenzio kwa kutoa ushauri kwa mwanaume anaekutaka au kumwambia mkewe kwa namna yeyote ile hata kama ni ku-form urafiki wa kizushi (sio kwenda na kudai mumewe anakutaka, hapana) bali kumtahadhalisha kuwa awe muangalifu na mwenendo wa mume wake na kama kuna kitu kinakosekana ndani ya nyumba kama vile romance,amani, upendo, ngono, n.k. basi ajaribu ku-restore vinginevyo ataletewa magonjwa, ikiwezekana mfundishe, muelekeze nini cha kufanya......najua mwanamke mjinga-mjinga atadhani unataka kumuibia mumewe lakini mwanamke muelevu atakuelewa na kukushukuru.

Kwa bahati mbaya umechelewa na hakuna kitu unachoweza kukifanya ili rafiki yako na mfanyakazi mwenzio ambae katika hali halisi ni Fuska ili waachane bila kukudhani kuwa wewe unawaonea wivu kutokana na wanavyopendana nakufanyiana mambo ambayo wewe umeona ni muhimu na kuyataja kama vile party, vifaa vya ndani n.k.


Nini cha kufanya-Kaa chini na rafiki yako na mueleze ukweli kuhusu huyo Baba (mfanya kazi mwenzio) kuwa ametelekeza familia yake kwa ajili ya huyo rafiki uliyemuunganishia......unaweza kusema ulimsakizia kwa vile wewe hukutaka kuendelea kusumbuliwa na huyo mwanaume lakini hukutegemea kama wangeanzisha uhusiano nakufikia hatua ya huyo jamaa kutelekeza mke na watoto wake.


Kwa vile unauzoefu na ndoa, familia yenye watoto uliowazaa mwenyewe na Talaka unajua wazi maumivu anayopata mke ikiwa atagundua mumewe anatoka nje ya ndoa, hofu ya watoto kuishi bila baba yao....hivyo pamoja na maelezo mengine muhimu tumia uzoefu wako huo kufikisha ujumbe kwa rafiki yako juu ya kutembea na mume wa mtu.....omba radhi kwa kuwaunganisha ikiwezekana.


Itakuwa ngumu na itamchukua muda mrefu kwa rafiki yako kuachia ngazi ikiwa amejenga mapenzi ya kweli na huyo mwanaume, inawezekana kabisa akamshawishi jamaa amuache mkewe ili amuoe yeye na hapo ndio utakapojisikia vibaya zaidi. Kwani itakuwa sio tu umesababbisha wawe wapenzi bali pia watakuwa mke na mume na wakati huohuo utajisikia unahatia kuwa umevunja ndoa ya mwanamke mwenzio kwa kumrusha mume wa mtu na rafiki yako.


Baada ya kuweka wazi kwa rafiki yako achana nao waendelee na mambo yao, Yeye kama mtu mzima atakuelewa, atatafakari na kufanya uamuzi wa busara. Endelea na maisha yako na watoto wako bila kuonyesha chuki juu ya uhusiano wao ambao sio halali.

Mungu akubariki na kila lililo jema!

No comments:

Umesoma hizi hapa